Mhubiri 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 4 (Swahili) Ecclesiastes 4 (English)

Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji. Mhubiri 4:1

Then I returned and saw all the oppressions that are done under the sun: and, behold, the tears of those who were oppressed, and they had no comforter; and on the side of their oppressors there was power; but they had no comforter.

Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; Mhubiri 4:2

Therefore I praised the dead who have been long dead more than the living who are yet alive.

naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua. Mhubiri 4:3

Yes, better than them both is him who has not yet been, who has not seen the evil work that is done under the sun.

Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo. Mhubiri 4:4

Then I saw all the labor and achievement that is the envy of a man's neighbor. This also is vanity and a striving after wind.

Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe; Mhubiri 4:5

The fool folds his hands together and ruins himself.

Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo. Mhubiri 4:6

Better is a handful, with quietness, than two handfuls with labor and chasing after wind.

Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. Mhubiri 4:7

Then I returned and saw vanity under the sun.

Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa. Mhubiri 4:8

There is one who is alone, and he has neither son nor brother. There is no end to all of his labor, neither are his eyes satisfied with wealth. For whom then, do I labor, and deprive my soul of enjoyment? This also is vanity, yes, it is a miserable business.

Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Mhubiri 4:9

Two are better than one, because they have a good reward for their labor.

Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Mhubiri 4:10

For if they fall, the one will lift up his fellow; but woe to him who is alone when he falls, and doesn't have another to lift him up.

Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? Mhubiri 4:11

Again, if two lie together, then they have warmth; but how can one keep warm alone?

Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi. Mhubiri 4:12

If a man prevails against one who is alone, two shall withstand him; and a threefold cord is not quickly broken.

Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. Mhubiri 4:13

Better is a poor and wise youth than an old and foolish king who doesn't know how to receive admonition any more.

Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini. Mhubiri 4:14

For out of prison he came forth to be king; yes, even in his kingdom he was born poor.

Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule. Mhubiri 4:15

I saw all the living who walk under the sun, that they were with the youth, the other, who succeeded him.

Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo. Mhubiri 4:16

There was no end of all the people, even of all them over whom he was--yet those who come after shall not rejoice in him. Surely this also is vanity and a chasing after wind.